Manchester United imejichomoa nafasi ya chini ya kundi lao katika Ligi ya Uropa kwa kupata ushindi usioridhisha wa goli 1-0 dhidi ya timu ndogo ya nchini Ukraine, ya Zorya Luhansk.
Zlatan Ibrahimovic alifunga goli pekee katika mchezo huo akiunganisha kwa kichwa shuti lililopigwa ovyo la Wayne Rooney.
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Old Trafford, Manchester United, waliutawala hata hivyo Zorya walionyesha kuwa tishio kidogo.
Zlatan Ibrahimovic akipiga kichwa mpira uliozaa goli
Mpira wa kichwa uliopigwa na Zlatan Ibrahimovic ukitinga golini
Shuti lililopigwa na Marcus Rashford likigonga mwamba na kushindwa kuingia langoni
0 comments:
Post a Comment