Makumi ya watalii wamekwama juu ya magari ya kutumia waya katika Mlima wa Alps nchini Ufaransa na kulazimu 45 kulala kwenye magari hayo usiku kucha, baada ya upepo mkali kusababisha hitilafu ya kiufundi.
Zoezi la uokoaji lilifanywa kwa watalii hao zaidi ya 110 kwenye magari hayo ya kukatiza juu ya mlima kwa kutumia kamba wakiwa juu umbali wa mita 50 katika eneo la Mont Blanc katika Mlima wa Alps.
Waokoaji wa mataifa ya Ufaransa, Italia na Uswizi jana usiku walitumia helkopta kuokoa watalii 65 kati ya 110 waliokuwa wamekwama, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Chamonix, Bernard Cazeneuve amesema.
Waokoaji wakiwa wanafanya kazi ya uokoaji kwa kutumia helkopta
Baadhi ya watalii waliookolewa wakiwa na furaha
0 comments:
Post a Comment