Mamlaka nchini Marekani imetoa wito wa kuondolewa sokoni kwa simu aina ya Samsung Galaxy Note 7 baada ya kuripotiwa kusababisha moto kutokana na kuwa hitilafu kwenye mfumo wa betri.
Kampuni kubwa ya Korea Kusini inayotengeneza simu hizo tayari nayo imetoa wito kwa watumiaji waliokwishanunua simu hizo kuzirejesha baada ya kuibuka kwa malalamiko kuwa zinalipuka moto.
Kwa mujibu wa kampuni ya Samsung, tatizo hilo limeathiri simu za Samsung Galaxy Note 7 milioni 2.5 duniani ambapo nchini Marekani pekee zipo simu milioni 1.
0 comments:
Post a Comment