Klabu ya Tottenham Hotspur inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) imepata majanga baada ya kujulikana kuwa inaweza kumkosa mashambuliaji wa klabu hiyo, Harry Kane kwa miezi mwili.
Sababu ya Kane kuwepo nje ya uwanja kwa muda huo ni majeraha ambayo aliyapata katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Sunderland ambapo alitolewa katika dakika ya 87 na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Baada ya zipimo, taarifa zinaonyesha kuwa alipata majeraha katika kifundo cha mguu na anaweza kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili lakini Tottenham bado haijatoa taarifa rasmi kwani inasubiri afanyiwe vipimo kwa mara ya pili na baada ya hapo itatoa taarifa rasmi.
Kama Kane atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mwili basi ataikosa michezo mitatu ya EPL dhidi ya Manchester City, Leicester City na Arsenal.