Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema leo Septemba 21.2016 amezindua rasmi kongamano la siku tatu la Chama cha Wataalam Wanasayansi wa Maabara za Afya ya Binadamu Tanzania (MeLSAT) unaofanyika katika hoteli ya St.Gaspar Mjini Dodoma.
Akihutubia wajumbe na viongozi mbalimbali wanaohudhuria mkutano huo, Dk. Kigwangalla amewataka wataalam hao kuzingatia weledi na taalum yao katika kupata majibu sahihi ya vipimo wanavyovifanyia kazi katika majukumu yao kwani wao ndio watu muhimu wa kubaini tatizo la mgonjwa.
Akisisitiza katika Kongamano hilo, Dk.Kigwangalla amebainisha kuwa huduma za maabara ni huduma nyeti sana katika tiba hivyo utamaduni wa Daktari kupima bila kupata vipimo vya maabara kwa sasa haukubaliki hivyo wangependelea zaidi wafanye uchunguzi katika maabara na hii ni lazima kwa madaktari wote kutumia Maabara katika shughuli zao.
Kongamano hilo la siku tatu lililoanza leo linawakutanisha wataalamu hao wa Wanasayansi wa Maabara zaidi ya 350 kutoka katika Kanda tano ikiwemo Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kaskazini, Kanda Kusini, Kanda ya Ziwa.
Tazama MO tv hapa:
0 comments:
Post a Comment