Manchester United imecheza mpira mbovu katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Uropa na kujikuta ikipata kipigo cha goli moja kwa bila kutoka kwa Feyenoord.
Jose Mourinho alifanya mabadiliko manane kutoka katika kikosi kilichofungwa na Manchester City na nafasi pekee katika kipindi cha kwanza ilipotezwa na Anthony Martial aliyepiga nje.
Zlatan Ibrahimovic aliingia kutokea benchi na kupiga nje ya goli mpira wa kichwa. Ilikuwa ni Nicolai Jorgensen, aliyeotea ndiye aliyeipatia goli Feyenoord akiunganisha krosi ya Tonny Vilhena.
Nicolai Jorgensen akifunga goli pekee katika mchezo huo
Paul Pogba aliyenunuliwa kwa paundi milioni 100 bado hajaweza kuonyesha cheche zake
Marcus Rashford akiruka kichwa ambacho hata hivyo mpira ulitoka nje
0 comments:
Post a Comment