Kocha Pep Guardiola ameibuka mshindi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya kocha rafiki yake wa zamani Jose Mourinho baada ya Manchester City kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Manchester United, Old Trafford.
Katika mchezo huo Kevin de Bruyne alifunga kiufundi goli la kwanza na Kelechi Iheanacho akafunga la pili baada ya shuti la de Bruyne kugonga mwamba katika mchezo ambao Manchester City iliutawala katika dakika zote 45 za kwanza.
United ilizinduka kabla ya kipindi cha mapumziko baada ya kipa Claudio Bravo kujikuta katika harakati za kuokoa mpira wa adhabu uliomkuta Zlatan Ibrahimovic ambaye aliisawazishia goli moja Manchester United.
Kevin de Bruyne akimpoteza mahesabu kipa David De Gea
Zlatan Ibrahimovic akiangalia mpira alioupiga ukitinga wavuni
Kocha Joes Mourinho akipeana mkono na kocha Pep Guardiola baada ya mpira kumalizika
0 comments:
Post a Comment