Kufuatia kocha wa Manchester City, Pep Guardiola kusema kuwa hatamchezesha mchezaji wa klabu hiyo, Yaya Toure mpaka wakala wake, Dimitri Seluk atakapomwomba msamaha kwa kumsema vibaya, wakala huyo amemjibu.

Seluk amesema kuwa haoni sababu ya kumuomba msamaha Guardiola kwani anachokifanya sio sahihi na kama anataka amuombe msamaha basi aanze Guardiola kumwomba msamaha aliye kuwa kocha Man City, Manuel Pellegrini.
“Nimwombe msamaha kwa lipi?, Guardiola ameshinda michezo michache na anajiona kuwa ni mfalme, ninaishi Ulaya kwahiyo naweza kusema lolote ninalolipenda, Guardiola hawezi nizuia,
“OK, nitamwomba msamaha Guardiola kama akimwomba msamaha Pellegrini kwa alichofamfanyia. Kama ni mwanaume wa kweli, hilo lisingetokea. Pellegrini alisaini mkataba mpya mwaka uliopita lakini ametolewa kwa ajili ya Guardiola,” alisema Seluk.