Usiku wa Septemba 13 2016 klabu ya FC Barcelona ya Hispania ilishuka katika uwanja wake wa Nou Camp kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kundi C wa klabu Bingwa Ulaya dhidi ya klabu ya Celtic ya Scotland, katika mchezo huo ambao Barcelonawaliishia kuiadhibu Celtic kwa kuifunga goli 7-0, Lionel Messi aliweka rekodi mpya.
Licha ya kuwa Lionel Messi ana rekodi nyingi katika soka, usiku wa Septemba 13 aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga hat-trick nyingi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hat-trick ya Lionel Messi dhidi ya Celtic inakuwa ni hat-trick yake ya 6 katika michuano ya UEFA Champions League.
Jikumbushe rekodi 10 za Lionel Messi katika soka
1- Kufunga goli nyingi katika hatua ya Makundi ya michuano ya klabu Bingwa Ulaya, amefunga jumla ya magoli 50.
2- Kufunga goli nyingi timu moja katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya, ameifunga Arsenal katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya mara 9.
3- Kuwa mchezaji pekee kuwahi kufunga goli 300 kwa haraka ukihusisha wachezaji kutoka Ligi 5 kubwa barani Ulaya, aliweka rekodi hiyo baada ya kucheza jumla ya mechi 334.
4- Kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kucheza jumla ya mechi 100 za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
5- Kuwa mchezaji mwenye umri mdogo pekee kufunga goli zaidi ya 400 akiwa na klabu moja, aliweka rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 27 na siku 300.
6- Kufunga goli nyingi ndani ya mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, amewahi kufunga goli 5 rekodi ambayo ni sawa na Luis Adriano.
7- Kuwa mchezaji pekee aliyewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or mara 5.
8- Kuwa mchezaji pekee aliyefunga magoli katika miji 23 katika michuano ya Ulaya.
9- Ni Mchezaji aliyewahi kuibuka mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika misimu minne mfululilizo, alifanya hivyo katika msimu wa 2008/9, 2009/2010, 2010/11, 2011/12.
10- Mchezaji pekee katika Ligi Kuu Hispania kuwahi kufunga hat-trick zaidi ya mbili katika misimu 7 mfululizo.
0 comments:
Post a Comment