Kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri, amesema kuwa kocha Jose Mourinho ni mtu mzuri, na misuguano yao yoyote ya nyuma imebakia historia.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza wataivaa Manchester United katika dimba la Old Trafford hapo kesho, huku makocha hao wakiwa na historia ya kukorofishana.
Jose Mourinho aliwahi kumuita Ranieri mtu aliyeshindwa wakati alipochukua nafasi yake Chelsea na pia alimtolea lugha chafu akiwa kocha wa Inter Milan.
Kocha Jose Mourinho amekuwa na tabia ya kubwatuka na kukorofishana na makocha wenzake
0 comments:
Post a Comment