Mwimbaji wa R&B Tanzania,Belle 9 amejitapa kwamba album yake ya Vitamin music itavunja rekodi za dunia pindi itakapotoka.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA radio,Belle amedai ameandika vitu vikubwa sana ambavyo mastaa wakubwa duniani hawajai andika kabisa.
“Albam yangu ya Vitamin Music itakuwa ni albam ya tofauti, itakuwa na vitu vingi fantastic, itakuwa na jumbe tofauti tofauti, kutakuwa na mada tofauti tofauti za mapenzi, maisha, hustling na pia ‘angle’ nyingi ambazo wasanii wengi duniani hawazigusi, kama nilivyosema vitamin music, nadhani hata Michael Jackson, Bob Marley hawajawahi kufikiria katika level hiyo“,alisema Belle.
0 comments:
Post a Comment