Timu ya Arsenal imetandaza soka safi katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza na kufanikiwa kupata ushindi wake wa nne mfululizo, baada ya kuifunga Chelsea magoli 3-0.
Katika mchezo huo Alexis Sanchez alitumia vyema makosa ya beki Gary Cahill na kufunga goli safi katika dakika ya 11, na kisha dakika tatu baadaye Theo Walcott akaongeza la pili kupitia pasi ya Hector Bellerin.
Shuti lililoachiwa na Alexis Sanchez likitinga wavuni na kuandika goli la kwanza kwa Arsenal
Mesut Ozil akifunga goli la tatu kwa Arsenal ambayo ilikuwa kwenye dimba la nyumbani la Emirates
Mshambuliaji nyota wa Chelsea Diego Costa alidhibitiwa vilivyo na beki Shkodran Mustafi
0 comments:
Post a Comment