September 23, 2016 jina la msanii Davido kutoka nchini Nigeria linazidi kuzungumzwa kila kona na safari hii sio kwa uzuri sana mtu wangu, maswali ni mengi juu ya ukimya wake kwenye kiwanda cha muziki. Hii imemfanya Davido kufunguka juu ya sababu za kupotea kwake.
Jina la Davido limekosekana kwenye vipengele vya tuzo nyingi zilizotolewa na kutajwa mwaka 2016, Ish hii imemfanya mmoja kati ya mashabiki wake kuandika kwenye Twitter juu ya nini kinachoendelea.
Sum of these artist only got nominated because @iam_Davido left the scene for 8months to work on new project wiv Sony/RCA .#FactsOnly.
Kwa bahati nzuri, Davido alimjibu shabiki wake na kukiri kuwa hastahili kuwepo kwenye list ya washindi au wanaowania tuzo mbalimbali kwa mwaka 2016.
0 comments:
Post a Comment