Urusi yazuiwa kushiriki kwenye Olimpiki ya walemavu

Kamati ya michuano ya Olimpiki ya walemavu, Paralympic, Jumapili hii imeizuia Urusi kushiriki kwenye michuano ijayo ya Olimpiki kwa kudaiwa kukiuka sheria za matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.

putin-mutko-1180
putin-mutko-1180
Hatua hiyo ilitangazwa na rais wa kamati hiyo, Philip Craven aliyeitupia lawama serikali ya Urusi kwa kuwaponza wana michezo wake. Alidai kukerwa na tabia ya Urusi kufikiria zaidi juu ya kushinda medali na si kufuata maadili.
Waziri wa michezo wa Urusi, Vitaly Mutko aliliambia shirika la habari la nchi hiyo, Tass kuwa wataukatia rufaa uamuzi huo kwenye mahakama ya kimataifa ya michezo ya Lausanne, Switzerland.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment