Dada hao wa Williams hawajawahi kushindwa kwenye mechi ya aina hiyo kwenye Olimpiki.
Wabaya wao walikuwa ni Lucie Safarova na Barbora Strycova wa Jamhuri ya Czech waliowashinda kwa seti 6-3 na 6-4.
Williams walishinda medali za dhahabu mwaka 2000, 2008 na 2012 wakiwa wawili. Kupoteza huko kunakuwa mwisho kwa Venus kwenye mashindano hayo mwaka huu.
Serena ataendelea na harakati zake za kuitetea medali yake ya dhahabu ya mchezo wa mmoja mmoja. Alishinda mechi yake ya kwanza Jumamosi dhidi ya Daria Gavrilova wa Australia.
0 comments:
Post a Comment