Bi Rose amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitaka Mamlaka hiyo kuweka saini ya mwombaji na mtoaji wa vitambulisho hivyo.
“Tumeanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais tangu mwezi Juni mwaka huu, hii inamaanisha kwamba vitambulisho vyote tulivyochapisha kuanzia mwezi Juni mpaka leo vina saini ya muombaji, saini ya mtoaji na tarehe ya kuzaliwa muombaji,” amesema Bi Rose.
Kaimu huyo amedai kuwa zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo hivyo inasubiri kuzinduliwa na Rais Magufuli atakayekabidhiwa kitambulisho cha uraia namba moja na baadaye vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wananchi wengine.
Bi Rose ameongeza kuwa Mamlaka hiyo itatumia taarifa za Tume ya Uchaguzi (NEC) zilizo katika vitambulisho vya kupigia kura na kuzihamishia katika kanzi data ya NIDA na mpaka sasa watanzania milioni 2.7 wamepatiwa vitambulisho hivyo na milioni 6.5 wamesajiliwa kwa ajili ya kupata vitambulisho hivyo.
0 comments:
Post a Comment