Maswali matatu ya ACT-Wazalendo kwa serikali ya Rais Magufuli


August 3 2016 Umoja wa vijana wa chama cha ACT-Wazalendo umekutana na waandishiwa habari Dar es salaam na kuzungumzia changamoto zilizopo katika sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja kitendo kilichofanywa na serikali kwa kuwafukuza wanafunzi wa Chuo kikuu Dodoma (UDOM) na hatimaye baadhi yao kurudishwa tena.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao Kitentya Luth ambaye ni mratibu wa vijanaACT-Wazalendo amesema…>>>‘Katika uamuzi huo wa kuwafukuza watoto wa kimaskini kutoka UDOM kukaibuliwa lugha za udhalilishaji kwa kuwaita Vilaza bila kuangalia athari za kisaikolojia
Sisi kwa nafasi yetu kama vijana tunalaani vikali udhalilishaji huo mbali ya kulaani tunaitaka Serikali ituambie na kutujibu masuala matatu yakiwemo‘ –Kitentya Luth
  1. Je, ni kweli tatizo lilikuwa Udahili ambao haukukidhi vigezo au ni ukosefu wa fedha baada ya wafadhili kujitoa kama tunavyosikia?
  2. Mliwezaje kuwapata wanafunzi zaidi ya 300 mkidai wamekidhi  vigezo vya kurudi chuo na tunafahamu 7000 walikosa sifa kwa matokeo yao kuwekwa hadharani?
  3. Serikali imewapeleka wanafunzi katika vyuo vingine, je, waliopelekwa walienda kuendelea na elimu waliyoanza awali au walikuwa na mwanzo mwingine
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment