WATU 6,000 WASHIKILIWA NCHINI UTURUKI KWA JARIBIO LA MAPINDUZI


Watu 6,000 wanashikiliwa nchini Uturuki kwa kuhusika na jaribio la mapinduzi lililokwama siku ya Ijumaa, na idadi yao inatarajiwa kuongezeka zaidi, Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Bekir Bozdag amesema.

Msako huo umehusisha kukamatwa kwa wanajeshi wa vyeo vya juu na majaji wapatao 2,7000, huku wanajeshi waandamizi wengine 50 wakikamatwa kwenye mkoa wa magharibi wa Denizli hii leo.


Waziri Bozdag ameelezea zoezi hilo la msako wa watu waliokula njama za jaribio la mapinduzi kuwa ni “Operesheni safisha”. Watu wapato 265 waliuwawa wakati wakipambana na wanajeshi waliotaka kufanya mapinduzi.
Kiongozi wa waasi Jenerali Erdal Azturk akiwa amekamatwa ambapo sasa anakabiliwa na kesi ambayo adhabu yake huenda ikawa ni ya kifo

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment