Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesafiri kwa ndege hadi Istanbul, baada ya kundi la jeshi kusema kuwa limetwaa madaraka ya nchi hiyo.
Rais huyo alionekana akiwa amezingirwa na raia wanaomuunga mkono wakimshangilia, ambapo katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni amesema kitendo hicho ni uhaini, na jeshi lazima lisafishwe.
Watu 60 walikufa katika mapambano ya usiku wengi wao wakiwa ni raia, ambapo wanajeshi 754 wamekamatwa.
Raia mwenye ujasiri akiwa amelala chini ya kifaru cha jeshi kukizuia kisiingie kuuteka uwanja wa ndege wa Ataturk.
Raia wa Uturuki wakiwakabidhi wanajeshi waliowashika kwa polisi baada ya kudhibiti mapinduzi ya kijeshi
Raia wakiwa juu ya vifaru vya jeshi wakishangilia baada ya kufanikiwa kuzima mapinduzi ya kijeshi
Hamna kupita kifaru hapa: Rai akiwa amesimama mbele ya kifaru kukizuia katika uwanja wa ndege wa Araturk
Raia aliyejeruhiwa akiwa amebebwa na wenzake kuwahishwa kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza
Raia aliyejeruhiwa akipakiwa kwenye kiti cha nyuma cha gari ili kuwahishwa hospitali kwa
0 comments:
Post a Comment