URENO YATANGULIA NUSU FAINALI EURO 2016 KWA MIKWAJU YA PENATI


Timu ya Ureno imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali za michuano ya Euro 2016, baada ya kuitoa Poland kwa mikwaju ya penati 5-3, kufuatia kumaliza kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.

Shukrani zimuendee Ricardo Quaresma aliyefunga penati ya ushindi kwa Ureno baada ya penati iliyopigwa na Jakub Blaszczykowski kuokolewa na Rui Patricio.

Katika mchezo huo Poland ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu za Ureno kupitia kwa Robert Lewandowski kabla ya Renato Sanches kusawazisha. Ureno sasa itavaana kati ya Wales na Ubelgiji.
                                Ricardo Quaresma akifunga penati iliyoipa ushindi Ureno
Beki wa Southampton Jose Fonte akishangilia huku akiwa amebebwa na Ronaldo mgongoni

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment