Ujio wa Usher Raymond Tanzania July 10 sema hutomuona kirahisi


Ugeni mwingine ambao Tanzania imekua ikitarajiwa kuwa nao toka juzi ya July 9 2016 ni ujio wa mwimbaji staa kutoka Marekani Usher Raymond ambaye anakuja Tanzania na moja kwa moja kwenda mbugani Serengeti.
Taarifa zilizosogezwa karibu yangu ni kwamba Usher anacho kibali cha kuwinda na uwindaji ataoufanya ni kwa kutumia Upinde na mkuki na ni kuanzia July 10 mpaka 19.
Usher anakua sio staa wa kwanza wa dunia kuja mbugani Serengeti nchini Tanzania, wengine wengi wameshawahi kuja akiwemo Mtangazaji Oprah Winfrey ambapo wengi wao huja lakini kwa kutotaka kutangaza au ijulikane, mpaka akiondoka ndio unaona kapost kwamba alikuwepo Tanzania.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment