Rwanda yasema haitamkamata Rais Omar Al Bashir wa Sudan atakapohudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika


Rwanda imesema haitamkamata Rais Omar Al Bashir wa Sudan atakapohudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika unaoendelea mjini Kigali.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Bibi Louise Mushikwabo amesema Rais Al Bashir atahakikishiwa usalama na ulinzi kama kiongozi wa nchi, na maswala yanayohusu kukamatwa kwake yatashughulikiwa na wale wanaohusika, lakini Rwanda haitamkamata. Amesema Rwanda itafuata kanuni za Umoja wa Afrika na sio za mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, kwa kuwa Rwanda si mwanachama wa mahakama hiyo.
Mwaka 2009 ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa Bw Al Bashir kutokana na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki yanayodaiwa kutokea Darfur kati ya mwaka 2003 na 2008.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment