Rais Francois Hollande wa Ufaransa ataongoza mkutano wa kujadili mashambulizi ya kigaidi na waziri wa mambo ya ndani kufuatia shambulizi la Alhamisi Mjini Nice lililouwa watu 84.
Bw. Hollande, ambaye amesema shambulizi hilo ni la kigaidi, tayari ameongeza muda wa hali ya tahadhari katika taifa hilo kwa miezi mitatu.
Alhamisi dereva mwenye lori aliligonga kwa makusudi kundi la watu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Bastille katika eneo la ufukweni la Promenade des Anglais.
0 comments:
Post a Comment