Viongozi wa umoja wa nchi za Afrika kwenye vikao vyake umepanga kutambulisha matumizi ya passport moja tu itakayotumika katika nchi zote za Afrika ili kurahisisha safari za ndani ya Afrika. Passport hiyo ya kielekroniki imepangwa kuzinduliwa wiki ijayo Kigali Rwanda.
Hii imekuwa ni mpango wa muda mrefu kuwa na passport moja katika bara la Afrika ifikapo mwaka 2020 ambapo ambapo utarahisisha kusafiri kwa waafrika wote bilioni 1.1 katika nchi zote 55 zaa bara la Afrika.
Mwenyekiti wa Tume ya umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma amesema mpango huo una lengo la kujenga umoja wa Afrika na kurahisisha safari za ndani na kuwezesha uhuru wa usafirishaji wa bidhaa na huduma ndani ya bara la Afrika.
0 comments:
Post a Comment