NG'OMBE DUME AMUUWA MPIGANAJI MAHIRI WA MCHEZO WA KUPIGANA NA FAHARI


Mmoja wa wapiganaji mahiri na ng'ombe dume (fahari) ameumizwa vibaya na kufa huku watu wakishuhudia, akiwemo mkewe ikiwa ni tukio la kwanza la kifo katika mchezo huo hatari nchini Hispania tangu kuingia karne hii.

Mwanamichezo huyo Segovia Víctor Barrio, 29, aliumizwa vibaya na ng'ombe huyo katika onesho ambalo lilikuwa linarushwa moja kwa moja kwenye televisheni katika mji wa Teruel huko Aragon, Mashariki mwa Hispania.

Mkewe aliyeshutushwa mno na tukio hilo Raquel Sanz, alikuwa miongoni mwa watazamaji walioshuhudia janga hilo katika mchezo wa kupigana na ng'ombe, wakati wachezaji wenzake wakikimbia kujaribu kumuokoa.
              Ng'ombe dume likimpiga pembe Segovia Víctor Barrio na kumuangusha chini
Wapiganaji wengine wa mchezo huo wakijaribu kumnusuru mwenzao waliyelala na kupoteza kabisa fahamu
Segovia Víctor Barrio akiwa amebebwa na wenzake ili kumuondoa uwanjani hata hivyo alishapoteza maisha
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment