Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ( mwenye kanzu ) akiwa eneo la tukio
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela ( mwenye kanzu ) akishirikiana na Kikosi cha Zimamoto kuzima moto na kuwapanga wananchi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alishiriki katika kuzima moto uliounguza bweni wanalokaa watoto yatima katika kituo cha Mgongo.
Moto huo ilioanza kwa hitilafu ya umeme umeteketeza mabweni 3 na kuunguza mali za watoto hao ikiwemo nguo, madaftari magodoro.
Kikosi cha zimamoto chini ya Mrakibu Komba kilifanya kazi ya ziada kuzuia moto huo usieneee majengo mengine. Wananchi wa eneo la Mgongo wamefanya kazi kubwa wakisaidiana na jeshi la zima moto.
Akizungumza na wananch,i Mh Kasesela ameahidi kuomba wahisani pia kuangalia uwezekano wa kuwasaidia waathirika wa janga hili la moto. Inakadiriwa watoto zaidi ya 45 wameathirika na moto huu ingawaje hamna majeruhi hata mmoja.
" nilipata taarifa nikiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ikabidi niache nije mara moja nafurahi kuona tumefanikiwa kuzima moto ingawaje umeleta madhara makubwa Pongezi ziwandee jeshi la Zimamoto pamoja na changamoto walifanikiwa kuzima moto huo" aliesema Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa wilaya alikutana na watoto na kuwapa matumaini serikali ipo pamoja nao. Serikali ya Wilaya ya irnga inawaomba wadau wajitokeze kusaidia watoto hawa mahitaji makubwa ni magodoro, blanketi na nguo hasa kipindi hiki cha baridi.
0 comments:
Post a Comment