BASTIAN SCHWEINSTEIGER NA ANA IVANOVIC WAFUNGA NDOA TENA KWA MARA YA PILI


Baada ya kufurahia kufunga ndoa yao ya kifahari waliyofunga kwenye ukumbi wa Jiji huko Venice siku ya jumanne Bastian Schweinsteiger na mkewe Ana Ivanovic wamefunga tena ndoa hapo jana safari hii ikiwa ni ndoa ya kidini.

Wanandoa hao wameamua kufunga ndoa tena baada ya kufunga ndoa ya kiserikali, wakaona hiyo haitoshi waongeze na ya kidini ili kujifunga zaidi katika kiapo cha ndoa takatifu, ambapo waliamua kuifunga kwenye kanisa la Misericordia huko Venice.
Kapteni wa timu ya taifa ya Ujerumani Bastian Schweinsteiger akiwa na mkewe mchezaji tenesi Ana Ivanovic baada ya kufunga ndoa ya kanisani jana
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment