Mwanzoni mwa mwaka 2016 Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea haki za wasichana kupata elimu, Rebeca Gyumi alifungua shauri mahakamani kupinga kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.
Maamuzi ya mahakama ni kwamba serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu kujipanga ili kuvirekebisha vipengele hivi tata ndani ya mwaka mmoja.
0 comments:
Post a Comment