ANDY MURRAY ASHINDA UBINGWA WA TENESI WA WIMBLEDON


Andy Murray amekuwa bingwa wa michuano ya tenesi ya Wimbledon kwa mara ya pili baada ya kuonyesha kiwango bora dhidi ya Milos Raonic wa Canada katika fainali.

Raia huyo wa Scot mwenye umri wa miaka 29, alimchakaza Raonic 6-4 7-6 (7-3) 7-6 (7-2) na kurejea kumbukumbu ya mwaka 2013 na kutwaa taji la pili la Grand Slam.

Murray anakuwa Muingereza wa kwanza kushinda mara mbili taji la Wimbledon kwa mchezaji mmoja tangu kufanya hivyo Fred Perry mnamo mwaka 1935.
                            Andy Murray akifurahia ubingwa baada ya kumshinda Raonic
                        Milos Roanic akimpongeza Andy Murray kwa kumgusa mgongoni 
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment