WANAWAKE HUTUMIA SIKU NNE KATIKA MWAKA KUTAFUTA NGUO ZA KUVAA TU

Ni kawaida kabisa kuwaona wanawake wakipoteza muda mwingi kupekua kabati wakijaribu kufikiria nguo gani ya kuvaa kiasi hata ya kuwafanya kuwa katika hali ya kupaniki.

Watafiti wameamua kufuatili muda wanaotumia wanawake kutafuta nguo ya kuvaa na kubaini hutumia karibu dakika 17 kwa siku, sawa na siku nne kwa mwaka wakitafuta nguo kabatini.

Hali hiyo ya wanawake kutumia muda mwingi kutafuta nguo ya kuvaa kabatini hufanya moja kati ya wanawake 10 kuchelewa kazini na moja kati ya 20 hushindwa kufika kwenye hafla kabisa.

Asilimia 21 ya wanawake wamekiri kuwa kitendo cha kuhangaika kuchagua nguo ya kuvaa kabatini huwasababishia ugomvi na wenza wao.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment