Video: Ulishawahi kufikiria kumeza samaki hai kama dawa? tiba hiyo imetumika kwa zaidi ya miaka 170


Wanasema imani ya mtu ndio ukombozi wake, ikiashiria kama utaamini basi utapona. Zipo nchi ambazo huaminika katika maswala ya matibabu  India pia ikiwemo, ila matibabu haya ya kuwamezesha samaki walio hai watoto pamoja na watu wenye matatizo ya kifua yamewashangaza wengi.
samaki insia
Huu umekuwa utamaduni wao wa muda mrefu huku wakiamini kuwa njia hii inaweza kurahisisha upumuaji kwa watoto na pia kwa wagonjwa wa Pumu  hii ndio tiba sahihi. Kila June familia mbalimbali hujumuika kwa pamoja ili kushiriki katika zoezi hili.
Mdomoni mwa samaki hao wanaweka dawa za asili zenye rangi ya njano na kuhakikisha anayepokea anameza vyote. Zoezi hili limekuwa likifanyika kwa miaka 170 ikiwa mwaka huu inakadiriwa zaidi ya watu laki moja walipokea tiba hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment