UJERUMANI YATINGA ROBO FAINALI EURO 2016 KWA KISHINDO


Ujerumani imeboresha nafasi yao ya kuweza kutwaa kombe la michuano ya Euro 2016 kwa kuichakaza Slovakia kwa magoli 3-0 huko Lille na kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Beki wa kati Jerome Boateng aliwapatia mabingwa hao wa dunia goli la kuongoza kwa shuti murwa la umbali wa yadi 25 kabla ya Mario Gomez kufunga goli la pili.

Julian Draxler, ambaye alitoa pande zuri la goli la pili alifanya matokeo kuwa 3-0 kwa shuti la karibu na mwamba baada ya mapumziko. Mesut Ozil alikosa penati katika dakika ya 14.
           Jerome Boateng akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la kwanza
                             Golikipa Kozacik akipangua penati iliyopigwa na Mesut Ozil
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment