June 22 2016 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amehutubia katika Jubilei ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliyofanyika katika ukumbi wa Benki hiyo, mtaa wa Mirambo Jijini Dar es salaam.
Katika hotuba yake Rais Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda mfupi usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa.
Rais Magufuli amesema zoezi hilo halina nia ya kuwakatisha tamaa watumishi wa umma na amewahakikishia watumishi wote wa umma kuwa serikali itaendelea kuajiri watumishi wapya na kuwapandisha vyeo waliopo kama kawaida mara baada ya kukamilika kwa zoezi, Rais Magufuli amesema……….
>>>’Serikali ninayoiongoza haina nia ya kuwakatisha tamaa wafanyakazi, lengo lake ni kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya, na ndio maana nimesema kwa kipindi cha mwezi mmoja hivi au hata mwezi mmoja na nusu, haitazidi miezi miwili, tusiajiri mtumishi yeyote serikalini’
>>>’katika kipindi cha mwezi mmoja hatutawapandisha vyeo wafanyakazi, ninaomba wafanyakazi waelewe hili, kwa sababu tukiendelea tutakuwa tunawapandisha vyeo hata wafanyakazi ambao hawapo, tunafanya ukaguzi wote tukishamaliza wafanyakazi wataendelea kupandishwa vyeo” amesema Rais Magufuli’:-Rais Magufuli
0 comments:
Post a Comment