TIMU YA MANCHESTER CITY YAMSAJILI ILKAY GUNDOGAN

Timu ya Manchester City imekamilisha mpango wa kumnunua kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan kwa kitita cha paundi milioni 21, na kumpa mkataba wa miaka minne.

Gundogan anakuwa mchezaji wa kwanza wa Manchester City kusajiliwa na kocha mpya Pep Guardiola tangu ajiunge na timu hiyo inayotumia dimba la Etihad.

Kiungo huyo wa kati mwenye miaka 25 anaondoka Borussia Dortmund baada ya kuichezea klabu hiyo mara 157.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment