Tamasha la mwaka la kula mbwa limeanza kusini mwa China, huku kukiwepo kwa pingamizi ndani ya nchi na kimataifa kupinga kufanyika tamasha hilo.
Wakati wa tamasha hilo jumla ya mbwa 10,000 na paka huuwawa na kuliwa nyama zao, wakati wote wa tamasha hilo la siku 10 huko Yulin, China
Wanaharakati wa haki za wanyama wanasema tamasha hilo linafanya ukatili kwa wanyama hao na tayari saini milioni 11 zimekusanywa kulipinga.
Maafisa wa Serikali za Mitaa za Yulin wamesema hawaungi mkono sherehe hizo, ila zinazoandaliwa na wafanyabishara binafsi.
Nyama ya Mbwa ikiandaliwa tayari kwa kuliwa wakati wa tamasha hilo
0 comments:
Post a Comment