Ni kawaida kwa wanawake kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana. Katika matukio mengi hali kama hizo, hutokana na mwanamke kutolainika sawasawa, hali hii inaweza kutatuliwa kwa urahisi kwa kuongeza muda wa kumchezea mwanamke(foreplay) au kutumia vilainishi vya ziada. Hata hivyo, iwapo maumivu hayakuweza kupungua, hizi hapa ni baadhi ya sababu, ambazo husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa:
Kukakamaa kwa misuli ya uke (Vaginismus): hali hii inasababishwa na mkazo katika misuli ya uke inayotakana na hofu ya maumivu au majeraha.
Matatizo ya shingo ya kizazi: Wakati mwingine uume unaweza kuingia ndani zaidi hivyo kugusa shingo ya kizazi. Iwapo mwanamke ana maambukizi huisi maumivu mara shingo ya kizazi inapogusana na uume.
Matatizo katika mfuko wa uzazi: Matatizo kama fibroids yanaweza pia kuwa sababu ya maumivu wakati wa ngono.
Maambukizi ya uke: aina yoyote ya maambukizi ya uke kama vile maambukizi ya fangasi inaweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana.
Kuumia uke: majeraha kutokana na sababu kadhaa mfano kuchanika wakati wa kujifungua au kuongeza njia katika msamba wakati wa kujifungua.
Endometriosis: Hii ni hali ambayo inasababisha tishu za mji wa mimba kukua nje ya mfuko wa uzazi, na hivyo kuchochea maumivu wakati wa kukutana kimwili.
Maambukizi kwenye funga nyonga(PID): Viungo kwenye nyonga vinaweza kupata maambukizi hivyo kusababisha maumivu wakati wa ngono.
Matatizo ya ovari: Matatizo haya ni pamoja na uvimbe kwenye mfuko wa mayai (ovarian cyst)
Wanakuwa waliokoma siku(Menapause): Wakati wanapokuwa wamekoma siku zao maumbile yao yanasinyaa na kuwa kavu, hivyo kuchochea maumivu wakati wa tendo la ndoa
Magonjwa ya zinaa: magonjwa ya zinaa kama malengelenge (herpes), masundosundo n.k, yanaweza kusababisha maumivu wakati wa ngono.

0 comments:
Post a Comment