Klabu ya Manchester United ya Uingereza imetenga dau la paundi milioni 30 ili kumnasa beki wa kati wa timu ya Villarreal raia wa Ivory Coast, Eric Bailly, ambaye anaaminika kuwa anakiwango cha juu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, alikuwa anafuatiliwa kwa karibu na timu za Manchester City, Bayern Munich na Arsenal katika siku za hivi karibuni lakini Manchester United ndio wamekuwa wa kwanza kutoa dau.
Bailly aliyeachwa katika kikosi cha Ivory Coast kilichoivaa Gabon hapo jana, pia timu za Barcelona na Leicester zilikuwa zikimfuatilia tangu Januari lakini Villarreal wanaimani kuwa anaweza akaenda Manchester United.
Beki Eric Bailly akiwa kibaruani dimbani
0 comments:
Post a Comment