Akitaja vigezo vya kushiriki Maisha Plus, Kaka Bonda, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa Maisha Plus alisema, “Tunachukua washiriki wenye umri wa miaka 18 hadi 26, walio na elimu na ambao hawajasoma kabisa, wawe raia kutoka nchi za Afrika Mashariki”
Maisha Plus kwa mwaka huu wa 2016 inatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi tano ambazo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ambapo mshindi atafadhiliwa wazo la biashara lenye thamani ya fedha ya kitanzania Milioni 30. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni ‘Vijana Ndio Ngazi’.
Usaili unaendelea katika mikoa mingine na nchi nyingine nje ya Tanzania. Vijana wametakiwa kusikiliza matangazo ya ratiba kupitia redio mbalimbali katika nchi shiriki, runinga ya Azam Two, mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na tovuti maalum ya mashindano hayo yawww.maishaplus.tv
Tunamalizia hivi kutoka kijiji cha Makumbusho Kijitonyama ulipofanyika usaili wa #MaishaPlusDar. Asanteni sana vijana wote mlioshiriki kwa wingi na wale wa mkoa wa Pwani na mikoa mingine mliojitokeza. Mliokosa nafasi kwa sababu ya kuchelewa ama sababu nyingine, poleni sana na karibuni msimu mwingine. Endelea kutufuatilia hapa mtandaoni na kupitia king’amuzi cha @azamtvtz kujua lini tutakua mkoani kwako. #MaishaPlusYaMwendoKasi #VijanaNdioNgazi
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment