LUIS SUAREZ APANDWA NA HASIRA BAADA YA KUJIKUTA HAYUMO KATIKA ORODHA YA WACHEZAJI WA AKIBA



Mshambuliaji Luis Suarez amepandwa na hasira na kukipiga ngumi kibanda cha wachezaji wa akiba baada ya kubaini jina lake halimo hata katika orodha ya wachezaji wa akiba wa Uruguay.

Suarez hakucheza katika mchezo huo ambao Uruguay ililala kwa goli moja kwa bila dhidi ya Venezuela na kuondolewa katika michuano ya Copa America.

Suarez alianza kupasha ili kuingia dimbani kujaribu kuokoa jahazi huku mashabiki wakimshangilia lakini kocha Oscar Tabarez alipofanya mabadiliko jina la Suarez halikuitwa.
               Luis Suarez akiwa amekata tamaa baada ya kutopata nafasi ya kucheza
                                    Solomon Rondon akifunga goli lililoizamisha Uruguay
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment