LeBron James ametangaza kutoshiriki katika michuano ya Olimpiki ya Rio nchini Brazil siku chache tu baada ya kutwaa ubingwa wa NBA na timu ya Cleveland Cavaliers.
Wakala wa James, Rich Paul amesema mshindi huyo wa medali za dhahabu mara mbili amekiarifu uamuzi wake huo chama cha Mpira wa Kikapu Marekani.
James (31) anaungana na wachezaji Stephen Curry na James Harden ambao nao wamejitoa kushiriki Olimpiki ili kupata muda wa kupumzika.
Stephen Curry akimzuia LeBron James katika moja ya mchezo wa fainali ya NBA
0 comments:
Post a Comment