Diamond asema 90% ya bifu za wasanii wa bongo zinazozungumzwa sio bifu kweli

Mkali wa muziki na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amesema 90% ya bifu ambazo zinazungumzwa na waandishi wa habari na kukuzwa sio bifu za kweli.
Simba

Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni, Diamond amesema kuna bifu nyingi zinakuzwa na waandishi wa habari lakini kiundani unakuta sio bifu kweli.

“Mimi nikiangalia karibu 90% ya wasanii wa Tanzania ambao watu wanadhani wanamatatizo, sio kweli wanamatatizo,” alisema. Diamond. “Kuna baadhi ya vyombo vya habari vinatumia hiyo nyenzo ili kutengeneza maslahi binafsi, mimi nakwambia ukweli kabisa, kwa sababu watu wengi ambao wanasema wanamatatizo hawana matatizo, wangekuwa wana matatizo tungesikia mtu akisema mimi nikikutana na flani nitamtia ngumi ya meno,”

Aliongeza, “Ukitaka kuamini kama ni uongo, juzi tukilisikia kuna bifu kati ya Shilole na Vanessa lakini kesho yake wakafanya show, hamna ugomvi,”

Pia muimbaji huyo amevitaka vyombo vya habari kuandika habari ambazo zina tija kwa wasanii na taifa kwa ujumla.

“So kama tulivyowaomba mwanzo, tunaviomba vyombo vyetu, na tunawaomba sana sana mtutengenezee umoja kwa wasanii ili tuweze kusaidia familia zetu. Watu wanapogombana tunatia vita katika sanaa, familia, watu kulogana, tuwapumzishe nao waganga wanachoka, tunapeleka hela za bure,” alisema Diamond.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment