UTAFITI WABAINI WANAWAKE WANAOJIPARA MNO WAKIENDA KAZINI HUPANDISHWA VYEO


Utafiti uliofanywa Marekani umebaini kuwa wanawake wanaotumia muda mwingi kujipamba asubuhi kabla ya kwenda ofisini, huwa waanapata mafanikio ya kupanda wadhifa kazini, kuliko wale ambao hawajali kujipara ama kuvaa nguo za kuvutia.

Utafiti huo unasema mafanikio ya kikazi kwa wanawake wenye umri wa miaka 24 na 32, unauhusiano na muda wanaotumia kujipodoa na kuvaa nguo za mvuto asubuhi, kwani wafanyakazi wanaovaa vizuri huwa na vipato vizuri na hupandishwa nyadhifa kazini.

Hata hivyo utafiti huo uliochapishwa na gazeti la The Huffington Post, unaonyesha kinyume na wanawake, wanaume hupata nafasi ya kupanda nyadhifa kazini kutokana na muonekano wenye mvuto wa asili.

Watafiti wa utafiti huo Jacyln Wong wa Chuo Kikuu cha Chicago na Andrew Penner wa Chuo Kikuu cha California, wamesema pia ni rahisi kupata ajira na kufanyiwa tathimini ya utendaji ya kupandishwa wadhifa kwa wanawake wanaojipara na wanaume wenye mvuto wa asili.
                                            Mwanamke mwenye cheo akipongezwa na wenzake 
                                   Kwa wanaume mvuto wa asili ndio siri ya kupanda cheo

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment