Sunderland imekwea kutoka timu tatu za chini mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada kutoka nyuma na kuifunga Chelsea kwa mabao 3-2.
Goli safi la Diego Costa lilifanya Chelsea iongoze lakini, Wahbi Khazri, akasawazisha kwa shuti zuri.
Nemanja Matic aliongeza bao la pili la Chelsea, kabla ya Sunderland kubadili mchezo katika kipindi cha pili kwa mabao ya Fabio Borini na la tatu la Jermain Defoe.
Jermain Defoe akiachia shuti lililoandika bao la ushindi kwa Sunderland
John Terry aliyesujudu akilambwa kadi nyekundu
0 comments:
Post a Comment