Bintiye Rais wa Zimbabwe, Bona Mugabe ajifungua mtoto wa kiume .Mtoto huyo wa kiume ni mjukuu wa kwanza kwa Rais Robert Mugabe.
Kulikuwa na ukosoaji mkuu nchini baada ya binti wa Mugabe kuondoka nchini na kusafiri Dubai kwa sababu ya kujifungua.
Duru zaarifu kuwa madaktari hawajamruhusu bintiye Mugabe kurudi nchini hadi mtoto huyo kufikisha mwezi mmoja kwa sababu za kiusalama.
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Februari mwaka huu ametimiza umri wa miaka 92 lakini lengo lake anasena ni kuishi miaka 100. Mwanasiasa huyo alizaliwa Februari 21, 1924.
0 comments:
Post a Comment