Fundi ujenzi mmoja huko Bristol nchini Uingereza, ameokolewa maisha yake na muuguzi ambaye aliyekuwa mapumzikoni baada ya kuchomwa kisu na kuachwa mtaani akingojea kifo chake.
Picha za tukio hilo la kutisha zinamuonyesha mtu aliyetapakaa damu akiwa amelala chali chini huku muuguzi huyo mwanamke akiwa amepiga magoti na kumsaidia kupumua mtu huyo ambaye alishaanza kukata pumzi.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema fundi huyo mwenye miaka 41, alianza kuishiwa na pumzi na mwili wake ulikuwa umeshalegea, hata hivyo muuguzi huyo alimsaidia hadi kilipokuja kikosi msaada wa dharura chenye vifaa tiba.
Muuguzi wa kike akimsaidia kupumua mtu aliyechomwa kisu
Watu wa huduma ya kwanza wakiwa wamefika na kuanza kutoa huduma
0 comments:
Post a Comment