Dogo Marcus Rashford ametakata wakati Manchester United ikitwaa nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Uropa kufuatia kuifunga Bournemouth mabao 3-1 na kuishusha daraja kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.
Mchezo huo wa jana ulishuhudiwa na mashabiki wachache katika dimba la Old Trafford, baada ya jumapili kuhairishwa kutokana na tishio la bomu ambapo baadaye ilibainika kuwa ni bomu feki.
Mkongwe Wayne Rooney alikuwa wa kwanza kuipatia Manchester United goli la kwanza, huku dogo anayekuja juu Marcus Rashford akifunga goli la pili kabla ya Ashley Young kupachika goli la tatu. Bournemouth walipata goli pekee baada ya Chris Smalling kujifunga.
Ashley Young akiachia shuti lililojaa wavuni na kuandia goli la tatu
Mashabiki wa Man U wakishinikiza kwa njia ya bango kocha Louis van Gaal aondoke
Asanteni kwa Kuja: Kocha Louis van Gaal akiwashukuru mashabiki
0 comments:
Post a Comment