Alfajiri ya May 7 nchi ya Uingereza kupitia jiji lake la London imeingia kwenye historia mpya kwa mara ya kwanza, baada ya kupata meya wa kwanza muislamu na asiye na asili ya Uingereza Sadiq Khan, Khan ametangazwa rasmi. kuwa mshindi wa umeya waLondon.
Khan ambaye alikuwa anagombea nafasi hiyo na wapinzani zaidi ya wawili, amefanikiwa kushinda umeya kwa asilimia 56.8 akifuatiwa kwa karibu na mshindani wake mkuu Tory Zac Goldsmith ambaye amefanikiwa kupata asilimia 43.2.
Baada ya kushinda Khan ambaye ana asili ya Pakistan kwa baba na mama ambao walihamia Uingereza miaka kadhaa iliyopita, alitoa kauli ya kwanza baada ya kutajwa mshindi wa umeya “Mtu kama mimi kuchaguliwa kuwa meya wa London !!! sikuwahi kufikiria kwa kweli, naahaidi nitakuwa meya wa watu wote wa London”
0 comments:
Post a Comment