Jose Mourinho atatangazwa kuwa kocha wa Manchester United katika saa 48 zijazo, na amedhamiria kunasa saini ya Zlatan Ibrahimovic ikiwa ni usajili wake wa kwanza akiwa Old Trafford.
Ibrahimovic ni mchezaji huru baada ya kuachana na mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa, Paris Saint-Germain, hata hivyo atahitaji paundi milioni 8 ya usajili na mkataba wa miaka miwili wa mshahara wa paundi 200,000 kwa wiki.
Nyota huyo raia wa Sweden mwenye umri wa miaka 34 ni aina ya wachezaji wanaohitajika na Mtendaji Mkuu wa Manchester United Ed Woodward, ili kuanza zama mpya za Mourinho, na inasemekana yupo tayari kuungana na kocha wake huyo wa zamani wa Inter Milan.
Kocha Jose Mourinho akiwa na Zlatan Inter Milan
0 comments:
Post a Comment