Muimbaji wa Ukraine, Jamala ameshinda shindano la mwaka huu la Eurovision Song Contest, lililofanyika jijini Stockholm, Sweden.
Nchi hiyo ilipata pointi 534 na wimbo wake 1944.
Australia ilishika nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 511 huku Urusi ambayo ilionekana kupendwa na wengi kwenye shindano hilo ikikamata nafasi ya tatu kwa pointi 491.
Ulikuwa na unahusu jinsi Josef Stalin alivyowafukuza watu wa kabila la Tatar kutoka kwenye jimbo lake la Crimea enzi za Soviet Union.
Wimbo huo umewakasirisha Warusi walioichukua Crimea kutoka Urusi mwaka 2014, na kusababisha kuwepo uhusiano mbaya kati ya nchi hizo mbili.
0 comments:
Post a Comment