ARSENAL YAIWEKEA NGUMU MANCHESTER CITY KATIKA DIMBA LA EDTIHA


Timu ya Manchester City huenda ikapoteza nafasi ya kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa majirani zao Manchester United baada ya Arsenal kupambana kiume na kulazimisha sare ya mabao 2-2 katika dimba la Etihad Stadium.

Magoli yaliyofungwa na Sergio Aguero na Kevin de Bruyne yaliipa Manchester City fursa ya kuongoza mara mbili katika mchezo wa nyumbani wa kumuaga kocha wao Manuel Pellgrini, anayeondoka baada ya msimu kumalizika.

Hata hivyo magoli ya Olivier Giroud na Alexis Sanchez yalitosha kuonyesha uwezekano wa kocha mpya wa Manchester City huenda akaanzia katika Ligi ya Uropa, na si Ligi ya Mabingwa Ulaya.
                                                         Kevin de Bruyne akishangilia goli alilofunga
                           Sergio Aguero akijipinda na kuachia shuti lililojaa wavuni

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment